Esri Eastern Africa Yazindua Ofisi mpya Tanzania
June 17, 2022 2022-06-24 7:32Esri Eastern Africa Yazindua Ofisi mpya Tanzania
Esri Eastern Africa Yazindua Ofisi mpya Tanzania
Esri Eastern Africa inafuraha kuwajulisha kwamba imefungua ofisi mpya Tanzania Mkoani Dodoma. Kampuni hii inahusika na mifumo ya teknolojia ya kijiografia (GIS). Dhumuni ni kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja. Ofisi hii inapatikana eneo la Kilimani, Ploti No.1103, Block AA Chinyoya.
Ofisi hii itawawezesha watumiaji wa mifumo hiyo kunufaika, kupata usaidizi wa karibu na mafunzo ya kina kutoka kwa wataalamu. Hivyo kupunguza gharama za usafiri kwani awali mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Arusha na Kenya tu.
‘’Ni furaha kwamba hii ni moja kati ya mikakati ya kampuni kutoa huduma kwa ukaribu Zaidi na wateja’’ . Alisema Clifford Okembo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Esri Eastern Africa.
Mifumo hii hutumika sana kwenye Sekta za Kiserekali, Huduma, Maliasili na Sekta za Kibiashara. Ni jukwaa madhubuti la ramani na uchanganuzi linalowawezesha watumiaji kuibua na kuleta maana ya kiasi kikubwa cha data kwa wakati halisi, na kuwaruhusu kutatua changamoto zinazotegemea eneo husika.
“Tunafurahi sana kufungua ofisi hizi mpya na hii inaonyesha dhamira ya Esri kusaidia jumuiya ya watumiaji wa GIS.” Alisema Clifford Okembo, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Esri Eastern Africa
Kuhusu Esri Eastern Africa
Ni kampuni ya kitaalamu ya kutatua masuala ya kijiografia ambayo huhamasisha, kuelimisha, na kuwawezesha wateja wetu kufanya kazi kwa masuluhisho ya GIS kwa ushirikiano na teknolojia za kijiografia zinazoongoza duniani kutoka Esri Inc, Trimble, CHCNAV, Harris Corporation na Airbus. Kwa habari zaidi tembelea www.esriea.com